Vigezo na Masharti

VIGEZO NA MASHARTI

Kwa kushiriki shindano hili unakubaliana na vigezo na masharti kama ilivyoainishwa hapo chini, na kwamba umesoma na kuelewa vigezo na masharti:

Kwa yeyote atakayependa kushiriki katika shindano hili, tafadhali zingatia vigezo na masharti hapo chini:

 1. Shindano hili ni mali ya Benki ya FINCA Tanzania na litaendeshwa na kituo cha Runinga cha TVE pamoja na kurushwa na kituo cha radio EFM.
 2. Mchakato wa kusajili watakaoweza shiriki shindano hili utafungwa tarehe, 27 Julai, 2018 kabla ya mda wa biashara kuisha (Saa Kumi na Moja Jioni – 05:00).
 3. Washiriki wanatakiwa wawe ni raia wa nchi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na awe na umri zaidi ya miaka kumi na nane (18).
 4. Shindano linakaribisha ushiriki wa mtu mmoja na sio kikundi.
 5. Kushiriki, mmoja anatakiwa awe ni Mteja wa Benki ya FINCA akiwa na Akaunti ya Akiba Binafsi.
 6. Endapo mtu si Mteja wa Benki ya FINCA, anakaribishwa kufungua akaunti ya Akiba Binafsi na Benki
 7. ya FINCA katika tawi lolote la Dar es Salaam yakiwemo (Victoria, Tegeta, Ilala na Airport) – angalia chini kwa maelekezo ya ku ka katika tawi la FINCA karibu yako au piga 0755 980 350 kwa maelezo zaidi.

 8. Ili kushiriki, mmoja anatakiwa awe ni mfanya biashara yenye Mtaji wa kiasi cha fedha za Kitanzania kuanzia Shilingi 10,000 – 5,000,000
 9. Kushiriki, mmoja anatakiwa aweke kiasi kisichopungua Elfu Ishirini za kitanzania (TZS 20,000) katika Akaunti yake ya Akiba Binafsi. Hii ni kwa walio tayari wateja wa FINCA na ambao watafungua Akaunti mpya na Benki ya FINCA.
 10. Baada ya kuweka akiba kwa ajili ya shindano, anayependa kushiriki atapaswa kuchukua fomu ya usajili katika tawi la Benki ya FINCA (Dar es Salaam) na kujaza taarifa zinazotakiwa pamoja na wazo la biashara.
 11. Wazo tajwa la biashara linatakiwa liwe kwa ajili ya kukuza, kuendeleza au kupanua biashara yake ambayo tayari inaendeshwa kwa mda usio chini wa miezi sita (6).
 12. Biashara tajwa inatakiwa iwepo na kuendeshwa katika Mkoa wa Dar es Salaam, Tanzania.
 13. Wazo la biashara linatakiwa liwe moja tu kwa kila anayependa kushiriki na si zaidi ya hapo.
 14. Watakao fanikiwa kupita watakua ni sehemu ya kipindi cha Runinga cha TVE ambapo watapewa
 15. mafunzo na wadau mbali mbali wa biashara nchini na watapata mitihani tofauti ambazo ndo zitakua sehemu ya shindano – watakaofanikiwa katika mitihani hiyo wataendelea kuwepo hatua kwa hatua hadi fainali.
 16. Jopo la majaji litakua na asilimia 80 ya maamuzi katika mitihani ambapo katika mitihani kabla ya fainali asilimia 10 itakua kwa washindanaji kutokana na asilimia nyingine 10 itakua kwa watazamaji kuchagua watakaobaki kutokana na mtazamo wao wa wazo zuri la biashara na ushabiki.
15. Picha au video za washiriki zitatutumika kwenye mitandao yetu ya kijamii tovuti na kutokea kwenye vipindi vya Runinga na Redio.

Kuzuiliwa Kushiriki Shindano hili

Mshiriki ataondolewa kushiriki katika shindano hili la Kuza O si na FINCA endapo ata;

 1. Kiuka vigezo na masharti hapo juu
 2. Atatumia lugha ya kuudhi
 3. Udanganyifu kama vile umri
 4. Kusababisha watazamaji wajisikie kuzarauliwa au kuudhiwa

Kusimamisha Shindano

Mwandaaji wa shindano hili ambaye ni Benki ya FINCA anaweza kusimamisha shindano hili bila taarifa pale anapoona inafaa, kuboresha, itakapobainika au kuamini umekiuka vigezo na masharti.

Maelezo ya mahali matawi ya Benki ya FINCA yalipo:

 1. 1. Victoria Branch (Tawi Kuu la Benki ya FINCA) – Barabara ya Old Bagamoyo – Victoria Area, Jengo la TAN House – Ground Floor
 2. Tegeta Branch – Barabara ya Bagamoyo – Basihaya – Jengo la Wema House – Ground Floor
 3. Airport Branch – Barabara ya Nyerere – Vingunguti – DL Plaza karibu na TRA
 4. Temeke Branch – Karibu na Soko la Stereo

Kuhusu zawadi kwa mshindi:

Zawadi ambayo itatolewa na Benki ya FINCA ni zaidi ya Milioni 10 za kitanzania ambazo zitatolewa kwa vipindi maalum tofauti. Mshindi ataendelea kupewa mafunzo na Benki ya FINCA na kuwa chini ya muongozo. Pindi pale Mshindi akifanikisha kila hatua ya maendeleo kibiashara Benki ya FINCA itatoa hela kwa ajili ya awamu nyingine ya kuwezesha biashara.

 
©2019 FINCA Microfinance Bank
Privacy Policy