Benki ya FINCA Microfinance ilianza kama taasisi ndogo ya kifedha hapa nchini ambayo ilikuwa ikijulikana kwa jina la FINCA Tanzania MFC Limited maarufu kama FINCA.

Hivi sasa benki hii imesambaa nchi nzima ikitoa huduma mbalimbali za kibenki, mmoja ya huduma ambazo imeipa FINCA umaarufu ni huduma ya FINCA Express. Finca Express ni huduma ambayo inatumia mfumo wa kisasa zaidi katika kuhakikisha mteja anaweza kuweka na kutoa fedha kwa usalama zaidi

Gazeti hili la MWANANCHI lilibahatika kufanya mahojiano mafupi na Meneja wa Huduma Mbadala za Kibenki, Eufrasia Asenga ili kupata undani zaidi kuhusu­ huduma hii:

FINCA Express ni kitu gani?
FINCA Express ni mtandao wa kibenki wa wakala unaotoa huduma za kifedha kwa wateja wake, ambapo huduma hii inaampa fursa mteja wa FINCA kuweka na kutoa fedha, kuuliza salio, kupata taarifa fupi ya akaunti, kuhamisha fedha kutoka akaunti moja kwenda akaunti nyingine, kulipa marejesho, kuingiziwa mkopo na kuweka fedha kwenye akaunti kwa kutumia mtu mwingine. FINCA ina mawakala hai wanaokadiriwa kufikia 137, ambapo hawa mawakala wanafanya asilimia 52 za miamala yote ya benk, wakati asilimia 25 ikipita kwa mawakala wa simu kupitia FINCA mobile na matawi yetu 25 yakifanya asilimia 23 tu ya miamala kupitia tela.

Vigezo vya kuwa wakala wa FINCA ni vipi?
FINCA ina malengo makubwa ya kuwawezesha na kuwainua wananchi ili waondokane na hali ya umasikini kwa kuwapa fursa ya kuwa mawakala wa huduma zetu za kibenki. Hivyo basi tumeamua kuweka vigezo vichache ili tu kila mtu aweze kupata fursa hii ambayo itamfanya afikie malengo yake hapo mbeleni, vigezo vikuu ni kama ifuatavyo, kwanza ili uwe wakala lazima uwe na uwezo wa kuwashawishi watu kuweka akiba, pili ili uwe wakala wetu tunashauri uwe na eneo maalum kwa ajili ya kundeshea shughuli hio na bila kusahau lazima uwe na umri zaidi ya miaka 18. Kama vigezo hivyo vikuu unavyo hapo ndipo tunapendekeza mtu yoyote hapa nchini afike tu karibu na tawi letu lolote hapa nchini ili aweze kupata kusajiliwa na kuwa mmoja wa mwanafamilia wa FINCA.

Mapokeo ya huduma ya benki ya FINCA yapo vipi?
Huduma ya FINCA Express kwa asilimia kubwa imepokelewa vizuri mno na wateja wetu kutoka sehemu mbalimbali hapa nchini Kwa sababu kuu mbili. Mmoja usalama wa fedha zao ambao umetokana na mfumo wa kisasa tuliouanzisha wa kutumia alama za vidole (Bayometria), ambayo inamuwezesha mteja wetu wetu kuweka na kutoa fedha zao kwa usalama zaidi. Pili mfumo huu ni rafiki sana hakuna haja ya kujaza fomu, miamala inakamilika ndani ya sekunde chache (real time) risiti inatolewa kwa kila muamala, hakuna namba ya siri ambayo mara nyingi wateja wanasahau au kutumiwa vibaya na ndugu/ rafiki wa karibu, au kadi ambayo inapotea au kuibiwa (kidole hakipotei, hakiibiwi).

Hebu tueleze upekee wa wakala wa FINCA.
Tofauti ya mawakala wa FINCA na wengine mawakala wetu tumewajengea mfumo ambao unawafanya wajisikie karibu na benk yetu. Wakala wetu wote wanapewa afisa maalum ambaye anakuwa anamtembelea kila wiki ili waweze kusikiliza changamoto za mawakala wa FINCA Express na kuzitatua kwa wakati ili tu wateja wetu wapate huduma ilio katika ufanisi wa hali ya juu. Pia wakala wetu wanapewa simu bure ambayo haina haja ya kuongeza muda wa maongezi kwa sababu katika kuhakikisha taarifa zinafika mapema tumeweka mfumo maalum ambao wakala anaweza kuwasiliana na afisa bila kuweka salio lolote katika simu hizo endapo wana tatizo au swali lolote kuhusu huduma zetu za FINCA.

Wakala wa kibenki wa FINCA anatoa huduma gani?
Huduma zitolewazo na mawakala ni pamoja na kuweka na kutoa fedha, kuuliza salio, kupata taarifa fupi ya akaunti, kuhamisha fedha kutoka akaunti moja kwenda akaunti nyingine, kulipa marejesho, na kuwekewa fedha kwenye akaunti kwa kutumia mtu mwingine.

Je, mnamuhakikishia nini mteja katika suala la fedha?
Mteja anapewa risiti kwa kila muamala anaofanya, pia anatia saini kwenye kitabu maalum cha FINCA Express wakala, na miamala yote inakamilika papo kwa hapo (real time). Miamala yote ya kutoa fedha lazima iidhinishwe na mteja mweyewe kwa kutumia teknolojia ya bayometria (kutumia alama za kidole).

Je, tutamtambuaje wakala wa FINCA?
Mawakala wetu wote wa FINCA huwa wana kifaa maalum cha biometria ambacho humuwezesha mteja wetu kupata huduma zetu zote za kibenki pale anapoihitaji huduma hio na pia wakala wetu hutoa risiti maalum yenye taarifa za aliyefanya muamala wakati huo na risiti hizo hutolewa paop kwa hapo na kama mteja hakufanikiwa kupata risiti yake katika eneo hilo hilo la wakala tumeweka namba zetu maalum ambazo mteja anaweza kumfikia afisa wa FINCA muda wowote na kutoa taarifa.

Na pia FINCA hutoa elimu elekezi kwa wateja mara tu baada ya kujisajili katika tawi lolote hapa nchini, elimu hio huwezesha wateja wetu kujua mawakala wetu hupatikana wapi na wapi. Hata katika yale makundi maalum ya wateja wetu huwa wanapata nafasi ya kuonana na maafisa wetu kila mwisho wa mwezi na kupata semina maalum kuhusu huduma tunazotoa kupitia hizo semina pia wanapata fursa za kujua mtandao mzima wa mawakala wetu nchini.

Je, ni namna gani FINCA inapanua wigo wa huduma za kibenki?
Mfumo huu wa kutumia mawakala ni mfumo ambao umeisaidia benki kusongeza huduma karibu na wateja kwa gharama nafuu, awali bila mfumo huu, benki ililazimika kufugua matawi mengi ili kuweza kusogeza huduma kwa watja , ambayo igekuwa gharama kubwa sana na benk insingeweza. Lakini kupitia mfumo sasa benki imeweza kuongeza wigowa kutoa hudua za kibenki kwa wananchi wote waliopo mjini na vijijini kwa kusogeza huduma za FINCA karibu na makazi ya watu na biashara ambako huduma zakibenki hazipo.

Je, mnatumia njia gani kutoa elimu ya biashara?
FINCA inautaratibu wakuwapatia wateja elimu ya biashara na huduma zake kable ya kuwapatia huduma, hususani kwa wale wanaochukua mikopo. kushirikiana na viongozi wa Serikali za mitaa, FINCA inatoa elimu ya biashara na huduma za kifedha kwa wananchi.Serikali za mitaa ni miongoni mwa wadau wakubwa wa FINCA katika kuhakikisha elimu ya biashara kuhusiana na huduma za wakala wa fedha zinatolewa kwa wananchi wenye uhitaji kutokana na idadi na makazi ya wananchi hao ambao wengi wao wanaishi katika meeneo yaliyo chini ya mamlaka za Serikali za mitaa.

Mawakala kabla ya kusajiliwa kuwa wakala wanapatiwa mafunzo, ikiwemo ya biashara lakini pia kutoa huduma kwa waeja na kila wakala kumi waafisa wa FINCA ambaye kila siku huwatembelea na kufanya mikutano na kutoa elimu kwa wananchi wanaomzunguka wakala.

Kwa kutumia matangazo kupitia njia mbalimbali, mfano makala, matangazo ya radio na video fupi, mitandao ya Kijamii na tovuti, SMS nk .FINCA pia imejikita zaidi katika kutumia majukwaa ya mitandao ya kijamii katika kutoa elimu yenye kuhusiana na biashara ya huduma za wakala wa kifedha.

Je, mabadiliko ya teknolojia ya athari gani kwenu FINCA?
Mabadiliko ya teknolojia yametulazimu sisi kubadilika kutoka mfumo uliozoeleka hapo awali kwenda mfumo wa kidigitali ambao unatoa huduma kwa haraka na rahisi kwa wateja wetu, bila kuathiri lengo na dira ya FINCA na taratibu za uendeshaji wa shughuli za kibenki. FINCA ilizindua kampeni ya mabadiliko haya mwaka 2015 “Twende Kidigitali”.

Je, FINCA Express inakabiliwa na changamoto gani?
Changamoto tunazokutana nazo katika kuendesha FINCA Express ni watu bado hawafahamu kuwa huduma zinazotolewa katika tawi la benki la FINCA Microfinance benki pia zinapatikana kupitia wakala wetu wa FINCA Express.

Je, FINCA Express ina faida gani?
FINCA Express inaokoa muda na kuwafanya wateja watumie muda wao katika kuendeleza biashara zao. Inapunguza gharama , kwa kuondoa gharama za usafiri kuelekea katika matawi yetu. Inapunguza hatari ya kupoteza/kuibiwa fedha wakati wa kupeleka fedha katika matawi yaliyo mbali na wateja.