FINCA Microfinance Bank Tanzania Limited, ni mojawapo ya mtandao wa Benki za FINCA Impact Finance 20 zilizoenea Duniani, ambayo ilianza shughuli zake mnamo 1998 jijini Mwanza.

Tangu wakati huo imekua ikikukuwa kwa kasi na kueneza huduma zake nchini Tanzania, sasa hivi mtandao wa matawi zaidi ya 20 na zaidi ya mtandao wa mawakala zaidi ya 150.

Mabadiliko ya FINCA kuruhusiwa kuchukua amana

Mnamo Januari 2013, Benki ya FINCA ilianza kutoa huduma za amana. Hii ilifuata tukio la kihistoria katika sekta ya kifedha ya Tanzania wakati FINCA ikawa Microfinance ya kwanza kupewa leseni na Benki Kuu ya Tanzania ikiruhusu taasisi hiyo kupokea amana na kuendesha huduma za kibenki.

Kabla ya hapo, FINCA ilikuwa taasisi ndogo ya kifedha ikitoa mikopo midogomidogo kwa wajasiriamali wadogo haswa katika maeneo ya nje ya mji. Utoaji wa leseni na Benki Kuu kwa kweli ilikuwa hatua muhimu kuelekea ujumuishaji wa kifedha kwani FINCA ilileta zaidi ya wateja 72,000 wakati huo, haswa kutoka maeneo ya vijijini ya Tanzania katika sekta rasmi ya benki.

Mabadiliko kutoka kwa shirika dogo la kifedha ambalo halikuwa chini ya uangalizi wa Benki Kuu mpaka kuwa benki kamili inayosimamiwa na Benki Kuu pia iliona utamaduni wa kuokoa unaokua ndani ya soko letu kuu kwani jamii ilifaidika na ufunguzi wa Akaunti na taratibu za usimamizi ulio rahisi na salama.

Suluhisho zetu za kifedha zinalenga kuipa jamii msaada katika kufikia malengo yao ya biashara na ya kibinafsi. Kwa kuongeza, suluhisho zetu za Mkopo zinalenga kukuza pia sekta ya viwanda na kilimo ambayo ni uti wa mgongo kwa uchumi wa Tanzania

Njia zetu nyingi za huduma mbadala wa kibenki ni pamoja na huduma za kibenki kwa simu ya mkononi na mawakala wa Benki zimeundwa kuwapa wateja urahisi, usalama na kuridhika wanapohitaji fedha zao.

Benki ya FINCA imekuwa mtoa huduma anayeaminika wa kifedha nchini Tanzania kwa miaka 20 iliyopita na imepanga kudumisha viwango vyake vya kuwajibika vya kibenki wakati inaendelea kuwahudumia na kuwawezesha Watanzania kwa ujumla.

Kuwekeza katika teknolojia, Benki ya FINCA inamiliki teknolojia iitwalo Digital Field Automation (DFA), ambapo inawawezesha Maafisa wa Benki kufungua Akaunti, kufanya maombi ya mkopo, kupata alama za mkopo na mwishowe kutoa mkopo bila mteja kutembelea tawi la FINCA.

Teknolojia haina karatasi na hutoa huduma za kibenki za papo hapo nje ya Tawi, hii inatupa makali ya uzoefu wa wateja kwani katika ulimwengu wa teknolojia ya kifedha wakati ni muhimu katika kuwahudumia wateja.